FREEMASON NI AKINA
NANI?
Swali hili limekuwa
likiulizwa na mimi binfsi mara kadha tangu na baada ya kuanza kuchapisha makala
zangu kwenye gazeti la Mtanzani, nimekuwa nikiulizwa swali hili. Ni swali
ambalo muulizaji hulidhani ni jepesi tu na lenye majibu ya haraka haraka,
lakini ukweli ni tofauti kabisa.
Kwanza kubaliana na
mimi kuwa tunao freemason wa aina mbili kote duaniani. Kuna jumla ya
wanamasonia wanao karibia milioni sita kote duniani, ambao kama nilivyo sema
tunaweza kuwagawa katika makundi mawili tu.
Kundi la
Kwanza ni Freemason wanao onekana (Visible Freemason)
Kundi la Pili
ni Freemason wasio onekana (Invisible Freemason)
Asilimia tisini na
tani mpaka tisini na nane (95-98%) ya freemason wote duniani wapo kwenye kundi
la pili 'Visible Freemason' na Asilimia tano mpaka mbili (2%) ya freemason wote
ni Invisible freemason.
Hivyo basi mpaka
utakapo yaelewa makundi haya mawili ya kimasonia ndipo utakapo weza kuja na
tafsiri sahihi au definition ya freemason.
Definition au
tafsri inayotumika kwa sasa kuhusiana na freemason sehemu mbalimbali duniani
imeegemea kwenye kundi la kwanza la Visible Freemason. Tafsiri hiyo ni sahihi
kabisa lakini tafsiri hiyo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.
Tafsiri nyingi
kuhusiana na freemason zinawataja kama (1) kikundi au taasisi au jumuiya (2)
Ambayo asili yake ni kutoka kwa wajenzi wa zama za kati Ulaya (4) Ambayo sasa
inawakaribisha wanachama ambao hawana taaluma ya ujenzi kujiunga (5) Aambayo
inajihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii.
Hayo kwa uchache
utayakuta kwenye tafsiri nyingi za sasa kuhusiana na freemason, lakini kama
nilivyo sema huo siyo ukweli wote kuhusiana na freemason.
Ukitaka kuwafahamu
freemason vyema, watizame kama mfano wa jengo zuri lililo nakshiwa vizuri.
Jengo linapokamilika kujengwa, hufatiwa na kupakwa rangi na kutiwa nakshi
mbalimbali. Visible Freemason ni kama nakshi juu ya jengo, ni kama mauwa mazuri
kwenye ukuta wa jengo, halafu Invisible Freemason ndiyo haswa jengo lenyewe.
Hivyo ni wazi utafanya makosa makubwa ya kimsingi utakapo litafsiri jengo kwa
mujibu wa mauwa yaliyo chorwa juu ya ukuta wake, ni lazima tukwangue mauwa
yale, rangi yenyewe, halafu ndipo tutakapo kuta jengo lenyewe limejengwa na
kitu gani, juu ya kitu gani na muhimu kabisa kwa madhumuni gani.
Hivyo basi Visible
Freemason wanatumika kama ngao dhidi ya Invisible Freemason, lengo na kazi yao
ni kuyafinika yale ambayo yanafanywa na Invisible Freemason.
Jesse Jackson, huyu
ni mfano mzuri wa Visible Freemason
Nadhani huyu sote tunamjua, Mtanzania, freemason ambaye naye anawakilisha kundi la VISIBLE FREEMASON.
Mazzini na Mwenzake
Pike vinara wawili katika ulimwengu wa kimasonia, hawa ni Invisible freemason.
Pike na mwenzake Mazzin wanatajwa katika maandishi mengi kuwa ndiyo waandishi
wa mapinduzi makubwa Ulaya pamoja na vita vya I na II vya dunia na pia vita vya
III vya dunia vinavyo andaliwa hivi sasa.
Hivyo basi wakati
visible freemason wakiwaficha ngugu zao Invisible freemason kwa kuchangia
madawati, vifaa vya hosipitali, miundo mbinu na kazi mbalimbali za kijamii,
kaka zao Invisible freemason nyuma ya mapazia ya kiza kwenye mahekalu ya
kimasonia wanapanga na kutekeleza njama za kusimamisha utawala wa kishetani juu
wa wanadamu wote.
Jumuiya ya
kimasonia inayo madaraja 33 au 33 degrees, lakini asilimia 98 ya freemason wote
duania hawavuki daraja la 3 ambayo pia ni maarufu kama blue degrees. N a wengi
kati yao hawa asilimia 98 hawafahamu kabisa juu ya kuwepo kwa Invisible
freemasoni.
“Umasonia kama zilivyo dini zingine zote … unaficha siri zake isipokuwa kwa wateule, wajuzi na wenye hekima na inatumia maelezo ya uwongo ya nembo na alama zake kuwapotosha wale ambao wanaostahiki kupotoshwa ili kuficha ukweli, ambao ni nuru na (kutumia maelezo hayo) tunawaweka mbali na nuru hiyo” (Albet Pike, Morals and Dogma, uk. 104-5, 3rd Degree)
Pike hapi kaweka
nukta moja ya msingi kuwa Umasonia ni dini, ni dini ya nini, nitalijibu swali hilo
baadaye kwa urefu wake, ila ni dini ya kishetani kwa kifupi. Freemason kama
jengo la shule lengo lake ni kuuficha ukweli Fulani kwa watu Fulani, ambao hawa
ni lile kundi la freemason wanao fahamika, ambao wao ni kama mauwa mazuri juu
ya ukuta usio fahamika asili yake ni nini. Wateule wachache kama alivyo sema
Pike ndiyo makhususi siri hizo na mambo yake ya maajabu wanafunuliwa wanapo
yafikia madaraja ya juu kabisa.
Mathalani mwana
masonia ambaye anaona kuwa dini yake labda Ukristo au Uislamu ndiyo sahihi na
hawezi kuziacha basi huyu atabakizwa katika ile sehemu ya jumuiya inayoonekana,
huyu atakuwa ni mauwa kwenye jengo la kimasoni, huyu atakuwa ni yule freemason
anayo julikana na wanajamii na wala hafichi umasonia wake, na wapo wengi hawa
tunawaona kila mahala. Huyu hatofanikiwa kuufahamu ukweli labda autafute
mwenyewe binafsi lakini si ndani ya hekalu la kimasoni, huyu ni katika wale
ambao Pike anasema wanastahiki kupotoshwa. Lakini mtu huyu atajihisi anafahamu
kuwa anaujua ukweli kumbe la hasha, sivyo hivyo.
Utakumbuka Milton
Copper kwenye kitabu chake 'BEHOLD A PALE HORSE' ametuambia kuwa daraja
la 33 limegawanyika sehemu mbili, hivyo mtu huyu anaweza kafikishwa mpaka
daraja 33 lakini akawa ni miongoni mwa wale wanaofaa kupotoshwa, hivyo hatoujua
ukweli daima.
Hivyo freemason ni jumuiya ambayo inawagawanya wanachama wake katika makundi
mawili, kundi la wale wanao faa kuambiwa kila kitu na wale ambao wanastahiki
kupotezwa, hawafai kuambiwa kila kitu.
Freemason kutokana
na kazi zao kuna mahala utawasikia wakifahamika kama BABILON BROTHERHOOD, BIG
BROTHER, AU ILLUMINANTI, lakini majina haya siyo ya kwao, majina haya yanakuja
kutokana na aina fulani fulani za shughuli zao chafu za kimataifa walizo pata
kuzifanikisha au wanazo lenga kuzifanikisha na shughuli hizo asili yake ni za
kale zaidi kuliko freemason yenyewe.
Freemason imekuwa ikitajwa kwenye maduara ya majina hayo hapo juu na mfano wa
hayo si kwavile wao ni 'WACHEZAJI MAHIRI' kwenye mchezo mzima, bali zaidi
kutokana na ufahamu finyu wa asili ya matukio hayo na freemaso wenyewe.
Freemason katika hili duara la matukio makubwa na mazito ya kidunia kitu kidogo
mno, au ni sehemu ndogo sana kwenye duara la nyuzi 360.
kaka unaniogopesha unapo sema kuwa freemasonry ni kitu kidogo sana, mbona wao ndiyo wanao tawala dunia, bado sijakuelewa hapo, hebu nieleweshe hapo vyema.
ReplyDeleteKaka hata mimi ninawali kama hilo hilo hapo juu naomba muongozo wako tafadhali
ReplyDeletekaka eti nikitaka kujiunga na hawa jamaa nifanye nini?
ReplyDeleteKaka salim kwanza nikupe hongera kwa hili, ningependa kujua eti nikweli freemasonry wanakula nyama za watu? Na je ukitaka kujiunga ni lazima utoe kafara ndugu yako au watu wako wa karibu.
ReplyDeleteKwa hiyo kaka unamaanisha kuwa Ande chande yeye ni visible freemasonry na hafahamu chochote juu ya invisible freemasonry?
ReplyDeleteEti kaka je kANUMBA ALIKUWA NI FREEMASONRY na wao ndiyo walio muuwa? Vipi kuhusu Sharo Millionea na je na yeye alikuwa freemasonry na wao ndiyo walio muuwa? Na Diamond Je ni freemasonry, Je Mzee Ali Yusuph pia ni freemasonry?
ReplyDeleteHabari yako ndugu msomaji,
ReplyDeleteUkweli wala sikuogopeshi, ispokuwa huo ndiyo ukweli halisi, kuna msemo maarufu wa kiswahili usemao 'waona vuma baharini papa lakini ...'
Freemasonry ni sehemu ndogo sana kwenye mtandao huu mpana wa Babilon brotherhood, lakini inayo nafasi muhimu na ya kipekee kwenye mtandao wenyewe.
Nafasi ya freemasonry kwenye mtandao huu ni sawa na nafasi ya tofali katika jengo, kila tofali kwenye nafasi yake ndipo yanapo kamilisha jengo, na ndivyo walivyo freemasonry.
Mtandao huu ni mpana unahusisha tasisi za kitaifa na kimataifa, mashirika ya umma na yale ya watu binafsi, makampuni, familia, watu binafsi na mengine na mengine.
Lakini wote hao, muundo wa mtandao ni kama Jengo la Piramidi, ni lipana mno chini, na jembamba kadiri linavyo kwenda juu,hivyo kuna tasisi au mashirika, au makampuni, au familia au watu binafsi kwenye mtandao huu ambao nafasi yao ni chini kabisa, wengine wapo katikati na wengine juu kileleni.
Visible freemasonry ni miongoni mwa wale waliopo chini kabisa, wakati ndugu zao Invisible freemasonry wakiwa juu kileleni.
Itakuwa vyema kabla ya kuulizwa swali ukajitambulisha hata jina lako, nadhani aliyeuliza swali hapo juu alikuwa akimaanisha kuwa *ninaswali* na kama hivyo ndivyo, basi thani nitakuwa nimeshamjibu.
ReplyDeleteNdugu yangu uliye uliza ni namna gani unaweza kujiunga na hawa freemasonry, ningependa uniulize tena swali hilo baada ya mimi kutupia post zingine kadhaa kuhusiana na freemasonry, halafu tuone kama bado utakuwa na hamu ya kujiunga nao ama la, hivyo nitupie tena hilo swali baada ya wiki mbili hivi kutoka leo.
ReplyDeleteNdugu uliye uliza swali ikiwa kama moja ya masharti ni kuwatoa kafara na kama wanakula nyama za watu, ningependa kukujibu hivi,
ReplyDeleteKaribuni hivi nitaweka post ambayo ndani yake itaelezea tofauti ya Freemasonry na imani nyingine za kiza, sababu watu wengi wanashindwa kutofautisha baina ya yale wanayo yafanya freemasonry na washirikina wengine ...
Ndugu uliye uliza swali kuhusiana na Ande Chande, ningependa kushea na wewe kitu kimoja kuhusiana na freemasonry.
ReplyDeleteKutokana na maelezo ya Albert Pike kwenye kitabu chake maarufu ambacho ni kama muongozo kwa mason wote 'Moral and Dogma' ameutaja umasonia kama dini lakini mahala pengine akawataja 'Visible freeasonry' kama wasiyo stahiki kuambai ukweli.
Lakini pia freemasonry atakapofikia daraja la 28 kutokana na maelezo ya mwandishi mwingine William Cooper ni kwamba freemasonry ndipo anapoambiwa kuwa yale yote aliyo jifunza ndani ya umasonia kabla ya kufikia daraja hiyo ni uwongo na ayasahau na kuanzia hapo awemakini maana ndiyo mambo yanapoanza. Pia ni katika daraja hilo ndipo freemasonry anapo ambiwa kuwa utabiri uliofanywa na Jacob de Molei, aliyekuwa kiongozi wa Knights Templer kabla hajachomwa moto, iutabiri ule haukutokea bali freemasonry ndiyo walio tekeleza mauwaji ya Papa na Mfalme ili kutimiza maono yaliyo tolewa na Grand Master De Moley.
Lakini pia Cooper anatuambia kuwa daraja la 32 limegwanyika sehemu mbili kwenye kitabu alicho kiita 'Be Hold the Pale Hourse' kwamba kuna ambao wanafiki daraja la 32 na bado hawajui kitu, au bado hajaaminiwa kupewa fungu za siri hizo nzito, hivyo anapandishwa daraja lakini kama visible freemasonry ambaye hatofunuliwa siri za ndani za mtandao mzima.
Imenibidi kutoa maelezo hayo marefu ili kuweza kukujibu swali lako hivyo basi kutokana na swali lako inabidi kwanza kujua Chande yupo daraja la ngapi katika madaraj 33 ya freemasonry, lakini juu ya yote huyu ni visible freemasonry, na kazi yao ni kupaka mauwa juu ya ukuta kuficha madhila ya bwana wakubwa, na visible freemasonry ndiyo wanao stahiki kudanganywa kutokana na maelekezo ya kiongozi wao wa zama zote, Albert Pike.
Kuhusiana na hilo la wasanii wabongo kuhusishwa na zahama hili, ningependa munipe muda kidogo, na ndani ya wiki ijayo nadhani nitaweka post juu ya hili, lakini kutokukuweka njia panda ni kwamba hakuna kati yao aliye freemasonry, na vipi nimefikia kwenye hitimisho hilo, tukutane kwenye blog hii hii nitakupatia 'details'
ReplyDeleteumenigusa sana....tangu mwanzo sikutaka ku coment ila kwa kweli upo vizuri kwenye "quotes"
ReplyDelete