TUENDELEE NA SEHEMU YETU YA PILI YA HADITHI YETU ...
JE HILI
LINATOSHA KUMFANYA KANUMBA AWE NI FREEMASONRY? KWA SABABU ALIKUWA MAARUFU,
ALIKUWA NA KIPAJI, ALIKUWA NA MVUTO KWENYE JAMII NA ALIKUWA NA USHAWISHI WA
KIPEKEE KWENYE JAMII KUTOKANA NA KAZI ZAKE, JE HILI LINAWEZA KUMAPATI HIYO
TIKETI YA UMASONIA?
FREEMASON
WAPO MAKINI SANA KATIKA KUMPATIA MTU UANACHAMA KWENYE JUMUIYA YAO, KUNAZO HATUA
MAHUSUSI AMBAZO WAO INABIDI KURIDHIKA NAZO JUU YAKO WEWE KABLA YA KUKUPATIA
UANACHAMA KWENYE JUMUIYA YAO. LAKINI BADO UNAWEZA KUWA NA SIFA ZOTE HIZO NA KWA
WAO BADO UKABAKIA KAMA ZANA WATAKAYO ITUMIKIA KUFANIKISHA MAMBO YAO MAHUSUSI
BILA KUKUPATIA UANACHAMA, HIVYO UNAWEZA UKATUMIWA NA FREEMASONRY KATIKA
SHUGHULI ZAKO ZA KILA SIKU BILA WEWE MWENYEWE KUWA NI FREEMASONRY, NA UNAWEZA
KUTUMIWA KWA KUJUA AU KUTOKUJUA.
TUNAYO MFANO MZURI KWENYE HILI JUU YA WANAMUZIKI NA
WASANII WA KIMATAIFA AMBAO WAO WANATUMIKA KWENYE KAZI ZAO KAMA ZANA ZA
KUFANIKISHA MAUDHUI YA KIMASONIA KWENYE KAZI ZAO BILA WAO WENYEWE KUWA NI
FREEMASONRY.
KATIKA NCHI
ZA ULAYA KUNAYO MSEMO MAARUFU WANAO UTUMIA ‘SELL YOUR SELF TO THE DEVIL’
MSEMO HUU
ZAIDI UPO KWA WANAMUZIKI NA WACHEZA FILAMU HASA WAMAREKANI NA ULAYA, AMBAPO
MSANII ANAAHIDIWA KUWA KAZI ZAKE ZITAUZWA KWA KIWANGO CHA JUU, UATAPATA UTAJIRI
NA UMAARUFU LAKINI NI LAZIMA AIUZE ROHO YAKE KWA SHETENI KATIKA MISINGI NA
TARATIBU ZINAZO WIANA NA IABDA ZA KISHETANI, WANAMUZIKI WENGI WAMEFANYA HIVYO
NA KAZI ZAO ZIMEFANYA VIZURI MNO, LAKINI WAO SIYO FREEMASONRY.
Katika Picha hii, msanii Melyssa Ford alikuwa akizungumzia suala la wasanii kunaswa kwenye mtandaoo wa 'SELL YOUR SELF TO THE DEVIL' kwamba kitu hicho ni kweli kipo na wasanii wengi wanfanya hivyo kujipatia utajiri na umaarufu
MFANO WA
WANA
MUZIKI HAO NI EMINEM, RIHANNA, LIL WAYNE, FAT JOE, SAVEGE, BLACKSTONE
CHERRY, JAMIE FOX, THE GAME na wengine na wengine, utaona katika kazi za watu
hawa kuna vionjo, maneno, picha za video ambazo hazikupaswa kuwepo kwenye
nyimbo husika, na wala hazina maana yeyote ile kuwepo kwake, lakini zipi na kwa
upande mwingine, picha, maneno hayo au vionjo hivyo vinayo maana pan asana na
ujumbe muhimu sana kwa wafuasi wa kimasonia au ushetani. Huenda tukazitazama
kazi hizo wakati mwingine.
Mkataba huo unaandikwa na kusainiwa kwa kutumia damu yako mwenyewe iliyo tolewa mwilini mwako.
Hapa kwetu
hatuna hadithi ya ‘SELL YOU SELF TO THE DEVIL’ Ispokuwa tunayo hadithi
inayofanana na hiyo, ambayo ni uchawi na ushirikina, tofauti na ile ya Ulaya ya
kuiza roho yako kwa shetani, hii ya hapa kwetu ni kwa ajili ya kuupata utajiri
au kuwa maarufu kwa kulipa gharama ambayo maganga wa ushirikina ataona inafaa
kulipwa. Lakini kwa Ulaya moja ya masharti yake ni kuwa kazi zako zote unazo
zifanya lazima zibebe maudhui hayo ya kishetani.
Hili Kanumba alikuwa nalo lakini bado
halitoshi kunfanya awe ni freemason, tuna watu wengi maarufu na wenye ushawishi
kwenye jamii yetu ya kitanzania lakini kama Kanumba bado hatuwezi kuwaita ni
freemason.
Freemason
wanapo kutaka uwe mwanachama kuna ambalo wameliona utawafanyia kwa faida yao,
na hapa nazungumzia freemason zote mbili, freemason inayonekana (visible
freemason) na freemason isiyonekana (invisible freemason) wasomaji wa makala
zangu kwenye mtanzania wanafahamu kuwa hapa nazungumzia kitu gani. Karibu
asiliamia 80 mpaka 95 ya freemason wote duniani ni freemason wanao onekana,
mimi hawa nawaita ni mauwa yaliyo chorwa juu ya ukuta na kazi yao ni kuuficha
ukuta halisi usifahamike umejengwa na nini na wale wasio fahamu wakiona mauwa
hayo wanadhani ndiyo ukuta wenyewe, lakini siyo. Kwa hiyo hata Kanumba angekuwa
ni freemason basi angeingia kwenye kundi hili, freemason wanaonekana, au kwa
maneno mengine ni kundi hili ni ngozi ya kondoo kwenye mwili wa mbwa mwitu.
Je freemason
kuna ambacho wangeweza kuwa wanakihitaji kutoka kwa Kanumba mpaka wamtake
ajiunge nao? Kikubwa ambacho tunaona kingewafaa kutoka kwa ndugu yetu huyu ni
kazi na kipaji chake. Lakini je kazi zake hizi zinaubunifu wa kutosha, kutoka
kwenye maudhui mpaka kwenye kurikodi? Kama nilivyo sema awali moja ya kitu
ambacho mimi binafsi kinanifanya nisiwe mpenzi wa filamu za kitanzania zikiwemo
za ndugu yetu Kanumba ni ukosefu wa ubunifu na uhalisia wa filamu hizo.
Kwa
freemason tanzia ya filamu ni muhimu sana kwao kwa ajili ya kuiongoza jamii
kule wanapo taka nah ii ndiyo sababu Hollywood ni moja ya silaha zao kubwa na
yenye mafanikio makubwa mno. Kazitizame filamu hizi ambazo zimetoka Hollwood na
zenye maudhi ya kimasonia, Filamu zote za Will Smith ispokuwa the Bad Boys,
Seven years in Tibet ya Bradd Pitt, The Last Samurai ya Tom Cruise, The Affair
of the Necklace (2001), Bad Boys II (2003), Conspiracy Theory (1997), The End
of Days (1999), From Hell (2001), The Godfather Part III (1990), National
Treasure (2004), na Things to Come (1936) nimezitaja kwa uchache ila ni nyingi
mno. Ukitiza filamu hizo ambazo ni za kimasonia hasa, halafu ukilinganisha na
filamu zetu hapa nyumbani na hasa za ndugu yetu Kanumba tofauti yake ni kubwa
mno katika kila kitu.
HIZO HAPO JUU NI BAADHI TU YA FILAMU CHACHE SANA ZENYE MAADHUI YA KIMASONIA, UKIZITAZAMA FIALMU HIZI, UKIWATIZAMA WAAGIZAJI WAKE NA SIFA WALIZO NAZO KWENYE KAZI HIYO, MAUDHUI NA KIWANGO CHA UBORA KWENYE KAZI ZAO HIZO, KATU HUWEZI KUSEMA KAZI ZA KANUMBA ZILIFANYA NA USHAWISHI WA KIMASONIA, AU KAZI HIZO NDIYO MSINGI WA KUMSINGIZIA KUWA NI FREEMASON ...
Filam hizo zimejaa alama za kimasonia na mafundisho yake
na hata ujumbe wa siri ambao unaweza kufahamika kwa freemason tena wa daraja
flani tu. Kitu kama hicho hakipo kwenye kazi za Kanumba.
JAY Z KWENYE POZI LAKE LA KIMASONIA.
JAY Z KAWAAMBUKIZA WENZAKE
Ukimtizama mwanamuziki kama Jay Z, kumekuwa kuna tetesi
kama ni freemason, ingawa mwenyewe hajakiri hadharani lakini kazi zake, mavazi
yake, nembo na alama anazo tumia na mwisho kabisa nyimbo aliyo iachia mwaka 2009
zinamtambulisha kama ni freemason. Ukizitizama albam tatu za Jay Z, blue print
I mpaka III zimebeba maudhi ya kimasonia na inaelezwa kuwa kila albam moja
ilikuwa ni daraja moja baada ya jingine la kimasonia, yaani Jay , alikuwa
akipandishwa, kikawaida inamchukua freemason wa kawaida miaka mitano kutoka
daraja la I mpaka la III, lakini kwa mtirirko wa albam hizo tatu za Blue Print
ilimchukua Jay Z miaka 8 kufikia daraja la tatu, na kumbuka madaraja haya
matatu yanafahamika kama blue degrees sawa na majina ya albamu zote tatu,
kwasababu ya kwanza iliitwa Bluee Print I, halafu Blue Print II na mwisho Blue
Print III.
ALBUM TATU ZA JAY Z ZINAZO SIMAMA KAMA USHAHIDI WA JAY Z KUPANDISHWA DARAJA LA I MPAKA LA III YA KIMASONIA
Hivyo
tukimtizam Jay Z na hapo nimetaja kwa uchache sana kwani itahitaji makal zaidi
ya hii kumzungumzia huyo jamaana
shughuli zake za kimasonia, hivyo basi
tunapo mtizam Jay Z tangu anatokea Colombia Record ambayo nayo iko chini ya
mtandao wa kimasonia mpaka anaingia Rockeffeler ambayo nayo pia wanaimiliki
freemason na mpaka anaanza kuchukua digirii ya kwanza hadi ya tatu ya kimasonia
utaona si kitu ki rahisi au siyo kwa wepesi wepesi tu mtu anaweza kujiunga
kwenye mtandao huu wa kishetani duniani.
Mwingine anayehusishwa na mtandao huu ni Diamond, lakini mazingira ya kumuhusisha kwake hayana tofauti sana na yale ya Kanumba, lakini pia Diamondi mwenyewe amekiri kuwa yeye si mwanachama. Ushahidi unao jaribu kutajwa kama kigezo ni duni mno kushinda hata ule wa marehemu Kanumba. Kesi hiyo hiyo pia ni sawa kwa Mzee Yusuph na Marehemu Sharo, hakuna ushahidi wowote zaidi ya maneno ya mtaani kuwa watu hawa ni freemason, mahala pengine watu wamejaribu kuonesha picha ambazo baadhi ya wasanii wameonekana kutoa ishara za kimasonia, lakini ukiangalia picha hizo na mazingira yake utaoana kuwa hazihusiani na chochote kwa wao kuwa ni freemason.
Hii ni Video ya Rihanna, mazingira ya video yamezungukwa na michoro ya draft kwa kiasi kikubwa, lakini tunajua michoro hiyo inayo maana gani kwenye ulimwengu wa kimasonia, Rihanna alitakiwa afanye video yake eneo hilo, sababu hivyo ndivyo yule ambaye 'anamsimamia' alivyo taka iwe.
Jay Sean kwenye huu wimbo wake wa 'DOWN' akiwa na wacheza show wake wameifanyia kwenye sakafu ya KIMASONIA, hili halikuwa kwa bahati mbaya.
Lady Gaga kwenye hii show yake ya Live kwenye steji, mtizame mtu anaye cheza naye nembo ya nguo aliyo vaa, ni Piramidi lenye jicho moja, Lady Gaga imebidi alale kwa mgongo kuruhusu 'taa' kubwa ionekane, taa hiyo inasimama badala ya JUA, Yote haya hayakuwa kwa bahati mbaya.
Kwenye Vidio hii ya Rihanna unapoitizama kwa haraka huwezi kuona hicho Rihanna anacho jaribu kukiweka wazi kwa kila mtu kuona, na imefanywa hivyo makusudi sababu picha hii ilitakiwa ieleweke kwenye ubongo wako wa nyuma na siyo wa mbele, kwa vile huna mamlaka yeyote na kile kinacho ingia kwenye ubongo wa nyuma.
Wakati ubongo wako wa mbele umeona picha ya kwanza, ubongo wako wa nyuma unaona zaidi ya hapo, na hichi ndicho ubongo wako wa nyuma unacho kiona, ndicho Rihanna alicho ambiwa akuoneshe, hicho ni kichwa cha shetani mwenyewe, Maarufu kama 'BOPHOMET' au 'KICHWA CHA MBUZI' zitizame pembe zinazo tengenezwa na mikono yake, macho yanayo tengenenezwa na mifupa ya mabega, kisha pua na mdomo. Aina hizi za picha inabidi 'kufanyiwa editi' ili kuweza kutengeneza taswira iliyo kusudiwa.
HII HAPA TENA VIDEO NYINGINE YA RIHANNA, AMBAPO ANATENGENEZA UMBO LA KITU FULANI AMBACHO KITATAMBULIWA NA UBONGO WAKO WA NYUMA TU. UBONGO WA MBELE UTAONA KITU KINGINE WAKATI UBONGO WAKO WA NYUMA UTAONA KITU KINGINE TOFAUTI. HICHO HAPO JUU NI KICHWA CHA SHETANI MWENYEWE AMBACHO RIHANNA ANATAKA KIONEKANE KWENYE UBONGO WAKO WA NYUMA, KAMA ZILIVYO VIDIO ZINGINE NAYO HII IMEBIDI KUFANYIWA EDIT ILI KUWEZA KUFANIKISHA UMBO HILO.
AMBACHO UBONGO WAKO WA NYUMA UTAKINASA UNAPO TIZAMA VIDEO HII NI HICHO HAPO, KICHWA MBUZI AU KICHWA CHA BOPHOMET AU KICHWA CHA SHETANI
Hivyo kwa
kuokoa muda tu, aliyekuwa msanii wetu na ndugu yetu Steven Charles Kanumba
hafiti au haenei hata kidogo kwenye picha kubwa ya mtandao huu mpana wa
kimasonia eitha kitaifa au kimataifa. Nakutakia safari Njema ndugu yetu huko
uendako.
WAPENDWA TUKUTANE TENA HAPA HAPA KUENDELEZA MPAMBANO HUU
nc work broo
ReplyDeleteKazi nzuri sana tatizo la wabongo ndo hilo mtu akipata umaharufu basi ni freemason sasa hivi utasikia BaRaka mkinywa nae freemason
ReplyDelete