Thursday, May 23, 2013

JE KANUMBA ALIWAHI KUWA NI FREEMASON?

HII NI MOJA KATI YA HABARI NYINGI ZILIZO JARIBU KUMFUNGANISHA KANUMBA NA UFREEMASO,


JE KANUMBA ALIWAHI KUWA NI FREEMASON?

Kumekuwa na wimbi kubwa la watu maarufu hapa nchini kuhusishwa na mtandao wa freemason. Wanamuziki kadhaa wamekuwa wakihusishwa na jamaa hawa. Kifo cha Kanumba nacho hakija achwa nyuma kwenye hili, inasemwa naye alikuwa ni freemason na hata kifo chake chenyewe kimekuwa kikitajwa na baadhi ya watu kuwa kimesababishwa na freemason. Ama habari hizi zimekuwa siyo rasmi, kutoka kwa baadhi ya watu maarufu hapa nchini  kuhusishwa na freemason mpaka Kanumba na kifo chake.


Naomba kuweka wazi vitu viwili kwanza, mimi siyo mpenzi mkubwa wa filam za kitanzania na hii ni kwasababu ya ubunifu mdogo, maudhi yasiyo kuwa na uhalisia katika filam hizo na kasoro nyingine nyingi tu, hata Kanumba na filam zake sijawahi kuwa na kiu nazo, ingawa katika mazingira flani flani nimepata kuziona filamu zake na kasoro nilizo zitaja hapo juu zimekuwa zikijitokeza. Hivyo Kanumba namfahamu kama wanavyo mfahamu watanzania wengi kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Pili Nimekuwa nikiandika makala za freemason na shughuli zao kimataifa kwa takribani miaka saba sasa na kazi zangu zimekuwa zikimgusa kila aliyepata kuzipitia. Hili kwa kiasi flani linanipa nafasi katika kuweza kulizungumzia hili la Kanumba na ufreemason.

Moja ya picha zinazo lenga kumtambulisha au kimakosa zinazo tajwa kuwa zinamtambulisha Kanumba kama freemason, ni kweli kuwa freemason wanayo naman yao ya kushikana mikono wakati wa kusalimiana, ‘hand shake’, lakini hiyo ambayo tunaiyona kwenye picha hii, katu hata kidogo siyo alama ya kimasonia, na salam hiyo hutolewa pale freemason wawili wanao fahamiana au wasiyo fahamiana wanapo kutana, lakini kwanza kabisa hiyo SIYO SALAM AU SIYO NAMNA AMBAYO FREEMASON WANATUMIA KUSALIMIANA, NA PILI ALIYESHIKANA MKONO NA KANUMBA HAKUNA USHAHIDI WOWOTE UNAO MTAJA KAMA NA YEYE NI MASON, HIVYO ALIYEWEKA PICHA HII KWA MAANA YA KUMTAMBULISHA KANUMBA KAMA FREEMASON KWA MSINGI WA KUSHIKANA KWAO MKONO HUENDA ALIKUWA AKIPOTOSHA KWA MAKUSUDI AU HAFAHAMU ANACHO KIANDIKA

Kwa watanzania wengi kutokana na uzoefu wengi kwenye kuwafatilia hawa jamaa na kazi zao, freemason ni kitu kigeni mno. Hii ni kwasababu watanzania wengi si wasomaji wazuri wa vitabu bali zaidi wasikilizaji wa nani kafanya nini na kupitia mistari miwili kwenye kurasa mbili tatu za mtandao na kujihisi tunafahamu hadithi nzima. Utakutana na watu wanakuambia ‘Kanumba bana, alikuwa ni freemason na wao ndiyo walio muuwa’ lakini ukimuuliza mtu huyu freemason ni nani au akina nani, anaanza kumumunya maneno, hana anacho kifahamu. Hivyo wengi hawajui hata hiyo freemason ni nini.
Maisha binafsi ya Kanumba siyafahamu akama ambavyo hawayafamu watanzania wengi, ispokuwa natumia uzoefu wangu mdogo wa takribani miaka saba kwenye kuwafatilia hawa jamaa na kuona kama Kanumba alikuwa anafit kwenye picha yao au la.
Picha hii nayo kimakosa inatumika kumtambulisha Kanumba kimakosa kama mfuasi wa freemason, kwa vile mikono yake imechora moja ya alama za kimasonia, kwanza ni uwongo, kwa vile alama hiyo hapo haijakamilika, pili kuna tafsri nyingi tu unaweza kuzipata kutokana na uwekaji huo wa mikono, tatu mbona hilo ni pozi tuu, mtu yoyote anaweza kuliweka, ki ukweli unahitaji kukifahamu kitu vizuri kabla haujakiandika au kukihusisha na kingine.

Sambamba na Kanumba pia tutizama wasanii wengine wanao tajwa na kuingizwa kwenye mkumbo huo hapa nchini, mmoja wa wasomaji wa blogu hii alipata kuniuliza swali kama Kanumba, Diamond na Mzee Yusuph ikiwa nao ni freemasonry, nikaahidi kuwa nitalijibu swali lake nah ii post ndiyo jibu lenyewe.
Tukiwa kwenye uwanja huo kuna vitu ambavyo ningependa tuvifahamu kabla ya kuuchambua ushahidi wenyewe kwa kina. Kuna hichi tunacho kiita freemason na kuna kitu kinacho itwa uchawi au ushirikina, UCHAWI UPO NDANI YA FREEMASONRY, LAKINI SI KILA MCHAWI AU MSHIRIKINA NI FREEMASONRY, UCHAWI AU USHIRIKINA UNAYO MASHARTI YAKE NA UFREEMASONRY NAYO INAMASHARTI YAKE, LAKINI MASHRTI YA UCHAWI NA YALE YA UMASONIA YANATOFAUTIANA KWA KIASI KIKUBWA MNO.
UCHAWI AU USHIRIKINA KATIKA HATUA FULANI HUHITAJI DAMU ZA VIUMBE MBALIMBALI MPAKA HATA BINADAMU, NA HASA MARA NYINGI KUTOKA KWA WATU WAKARIBU, KAMA WANAFAMILIA, NDUGU NA MARAFIKI. FREEMASONRY NAO HUHITAJI DAMU KATIKA IBADA ZAO, SIYO KATIKA KILA IBADA, HAPANA KATIKA IBADA MAALUM, ZA WANACHAMA MAALUM WA KIMASONIA, HASA WALE AMBAO WAPO DARAJA LA KUANZIA 28 NA KUENDELEA, LAKINI ZAIDI KUTOKA KATIKA DARAJA LA ILLUMINANTI, LAKINI FREEMASONRY HAWAHITAJI DAMU YA MWANAFAMILIA YAKO, AU NDUGU YAKO WA KARIBU AU RAFIKI YAKO KWA AJILI YA IBADA ZAO, HAPANA.
KWENYE SUALA LA DAMU YA MAKAFARA FREEMASONRY HUHITAJI DAMU MAALUM, DAMU YA MTU MAALUM, MWENYE SIFA FULANI FULANI ZA KIMAUMBILE, MWENYE DAMU AMBYO INASIFA FULANI PIA, NA MAKAFARA HAYO HAYAFANYI OVYIO, BALI KWA MISIMU MAALUMA NA NYAKATI ZAKE.

wengine hata nguo alizo vaa, ilimradi tu kilicho chorwa hakieleweki basi ni freemasonry, moja ya lama maarufu sana ya jamaa hawa ni fuvu la kichwa na mifupa, na wapo watu wengi wanao vaa mavazi na vitu vyenye nembo hiyo lakini hawatajwi kama ni freemason, ila sababu tuntaka kuuza gazeti letu au habari yetu basi chochote kinacho kuja hakieleweki tunakirushia huko, hiyo siyo sahihi, hata kidogo, fanyeni utafiti wa kutosha kabla ya kumlipua mtu.

Watu wengi wanasema Kanumba alikuwa ni freemasonry na alitakiwa kumtoa ndugu yake kafara na alipo kata basi umauti ulimfika, lakini kama nilivyo sema Freemasonry wanahitaji damu za watu, lakini SIYO KWENYE UTARATIBU KAMA UNAO TAJWA NA KUHUSISHA KIFO CHA KANUMBA.
FREEMASONRY HAWANA UTARATIBU WA MASHARTI AMBAO UNAWALAZIMISHA MMOJA AU IDADI FULANI YA WANAFAMILIA WAKO KUTOLEWA MUHANGA KWA WEWE KUENDELEA KUWA MWANACHAMA. LAKINI UCHAWI NA USHIRIKINA UNAYO MASHRTI KAMA HAYO KWA MTU ANAYE HITAJI KITU FULANI KUTOKA KWA WACHAWI HAO NA HASA KWENYE MASUALA YA KUUSAKA UTAJIRI.
SISEMI KUWA KANUMBA ALIKUWA NI MSHIRIKINA AU KAUWAWA KWA KUSHINDWA KUFUATA MASHARTI HAYO, HAPANA, HAYO NI MASIHA YAKE BINAFSI NA SIWEZI KUUSEMEA MOYO. NA HAYO YANAYO SEMWA NI MANENO YA MTAANI AMBAYO HAYANA USHAHIDI WOWOTE.
Kwa freemason, mtu yoyote anaweza kuwa mfuasi wa jumuiya hii, lakini kuna vitu vya msingi wanavyo tizama kabla hawajakupa uanachama. Ukiachilia mbali suala la kutambulishwa ndani ya jumuiya na mtu ambaye tayari ni mwnachama, lazima anaye omba uanachama awe ni mtu ambaye atailetea jumuiya faida flani. Faida hii inaweza kuwa katika tabia mbalimbali, lakini hasa napokuwa ni mtu mwenye jina kwenye jamii au ushawishi flani kwenye jamii huyu wanampendelea zaidi kwani ni rahisi sana kutumia ushawishi au utajiri wake katika kuwavuta na kulipamba jina la freemason kwenye jamiii.
nyota ni moja ya nembo zinazo TUMIWA SANA NA FREEMASON, Mungu akipenda huenda siku moja tukazizungumzia, hapa ni pale alipo tembelea Hollywood, na kama alivyo mtu yeyote angepiga picha kwenye maeneo kama hayo, lakini hii ndiyo inamfanya kuwa freemason? Kuna vyombo vya habari vilivumisha kuwa Kanumba alipata zawadi ya OSCAR???????????? KWELI, JAMANI MBONA TUNAKURUPUKA TU, TENA NI CHOMBO KIKUBWA SANA CHA HABARI KULICHORUSHA TAARIFA HIZO .... SIJUI ...?????

Je kanumba alikuwa kwenye ‘sell your self to the devil’ au alikuwa akishirikiana na waganga washirikina au alikuwa ni freemasonry kabisa, vipi kuhudu Diamond, Sharo je, Mzee Yusuph naye … tukutane tena hapa hapa kumalizia hadithi hii........










No comments:

Post a Comment