Freemasons ni jumuiya ya kale
mno, lakini kabla ya 1717 haikuwa ikifahamika rasmi kama Freemasons, ni
kiuhakika FREEMASONRY walikuwa ni waashi ambao walikuwa na utaratibu wao wa
namna ya kufanya ujenzi wao, walikuwa huru katika Ulaya ya zama za kati
wakiruhusiwa kuzunguka kila mahala kote duniani kama wangeweza, hawakuwa watu
ambao wakijihusisha na mambo ya maajabu kama wanavyo fanya Freemasons wa sasa,
mpaka pale mafundisho ya kipagani na uchawi kutoka Mashariki ya Kati kupitia
kwa Knights Tampler yalipochomokwa kwenye asasi hii ambayo awali haikujua
chochote zaidi ya ujenzi.
Hawa wajenzi wa zama za kati ndani ya
Ulaya walifahamika kwa jina la kazi yao, yaani masoni au kwa lugha yetu fundi
mwashi. Masoni walikuwa na utaratibu maalum wa kulinda siri hizi zinazo endana
na kazi yao, walikuwa na mahekalu yao, ambapo humo wanajumuiya walifundisha
maajabu na siri za kazi zao za ujenzi, lakini haya hayakufunuliwa kwa mtu baki.
Hivyo majengo mbalimbali ya ibada zama hizo, majengo ya kiserikali, makasiri ya
kifalme na nyumba za watu binafsi wenye ushawishi wa kiuchumi katika jamii
zilijengwa na watu hawa, masoni. Hii ndiyo maana Ulaya ya zama hizo
haikunufaika na maarifa haya kwa haki yake kwa vile haikuwa elimu aliyo pewa
kila mtu, bali ni kwa watu maalum na walitumia kwa majengo ya watu na vikundi
makhususi. Siku zote Freemasons walicho nacho ni cha kwao na ulicho nacho pia
wanataka wakichukue, daima wako kinyume na jamii inayo wazunguka, hivyo lolote
la kuinufaisha jamii halielezwi kwa wanajamii na wanafanya kila wawezalo
kuhakikisha wanajamii hawayapati maarifa hayo. Desturi hii wako nayo mpaka leo
hii, kila shida unayo iona duniani au maradhi ujue kuna tiba yake, kuna tiba ya
kansa, kuna tiba ukimwi kutaja kwa uchache, kuna suluhisho juu ya tatizo la
uchumi, kuna suluhisho juu mmomonyoko wa maadili lakini katu hayatatolewa, kwa
sababu wewe unaye soma kitabu hichi ndiye adui yao nambari moja!
Moja ya masalio ya majengo
yaliyo jengwa na MASONI wa zama za kati na ambayo pia lilitumika kama ofisi
yao.
Masoni hawa wa zama za kati katika
mahekalu yao walihifadhi zana zao za kazi, walipumzika humo na pia kula chakula
humo. Katika mahekalu hayo wanajumuiya walisimikwa katika madaraja ya kimasoni,
zama hizo kulikuwa na madaraja matatu tu, yaani Apprentices, Journeymen na
Grandmaster. Mason, hawa walikuwa wakijikusanya kama kikundi cha ushirika ili
waweze kupata kazi husika, walitambuana kwa salamu zao za siri na ishara
mbalimbali zilizo kuwa hazifahamiki kwa watu wengine.
Mwaka 1347 mpaka 1351 wakati Ulaya ikipambana
na janga la Black Death, mambo mengi yalikwenda mrama, taratibu na mipango
mingi iliharibika, shughuli za ujenzi zilipigwa marufuku, MASONI ambao walikuwa
na taaluma ya ujenzi nao walikuwa kwenye wakati mgumu.
Alama ya MASONI wa zama za
kati Ulaya inayo tambulisha eneo lao au ofisi yao ya kufanyia kazi, hapa ni
kabla jumuiya hiyo haijaingiliwa na kuigeuzwa na kufanywa kuwa FREEMASONRY.
Lakini wakati Ulaya inapambana na Black
Death, kitu kilicho pelekea mabalaa mengi likiwemo kwa jumuiya mbalimbali
kupigwa marufuku kabisa au kunyimwa kufanya kazi katika utaratibu walio uzoea,
takribani miaka 70, kabla ya Black Death, sehemu Fulani ya Ulaya ilikumbana na
kitimtim kingine ambacho athari yake ilisubiri kwa takribani miaka 70 iliweze
kuonekana, athari ya kile kilicho tokea mwaka 1307, sehemu Fulani kwenye jiji
la Ufaransa, ilisubiri mpaka balaa la Black Death lilipokuja na fursa mpya
ambayo kwayo, freemasonry ya leo ilizaliwa rasmi.
Lakini ni nini kilichotokea mwaka
1307, na kwa nini ilibidi kusubiri kwa takribani miaka sabini kupata fursa ambayo
kwayo freemasonry imezaliwa?
Punde
tutakifahamu hicho, lakini kwanza tutakuwa hatujatendea haki, tafiti mbalimbali
kama tutasimamia hapo kwamba freemasonry
ilizaliwa rasmi mwaka 1717, London Uingereza.
Hapana kama
nilivyo sema hapo juu ni kwamba 1717, freemasonry ilikuwa imezaliwa rasmi,
lakini si maanishi kuwa kabla ya 1717 hatukuwa na freemasonry.
kaka unaonekana uko vyema tafadhali endelea kutupa vitu
ReplyDeleteningependa kujifunza zaidi kuhusiana na ahwa jaamaa je niende wapi?
ReplyDeletesehemu inayo fuata itatoka lini kaka salimi, halafu big up sana
ReplyDeletethank you guys,
ReplyDeleteKama unapenda kujifunza zaidi kuhusiana na freemasonry tembelea blog hii kila wakati, utapata vitu tele tele hapa
sehemu inayo fuata ipo tayari just soon nitaiweka hapa kwenye blog yetu kila mtu aone.
ReplyDelete