Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Tuesday, May 8, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 4 (The Face of the Giants..)



Kote duniani, jamii mbalimbali wamekuwa na hadithi juu ya binadam wenye maumbo makubwa kupata kuishi kwenye jamii zao kwenye zama zilizo tangulia. Kwamba binadam hao walikuwa na maumbo makubwa na kimo kikubwa na urefu pia, na walikuwa ni majitu yenye nguvu.

Friday, April 27, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 3 (Time Reference..)


Time, nyakati ni kitu cha ajabu sana … tulipo ishia kwenye posti ya mwisho, itahitaji tujue kitu cha maajabu kinacho itwa ‘time’, bila kukijua hicho, hatuwezi kunyanyua mguu mmoja kwenda mbele.

Thursday, April 19, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep 2 (Binadam wa kwanza..)



Kwenye tamthilia ya Lost, Eko alipoamua ‘kumpokea’ Bwana, Lock alikuwa amevutika sana akataka kujua ni kwanini Eko kaamua hivyo, na Eko naye alitaka wafuasi kwenye ‘kanisa’ hivyo alikuwa na hamasa kumuelezea Lock, akamuambia, “Nitaanzia mwanzo”, Lock akasikiliza baada ya kitambo akamuambia Eko, “Sikujua kwamba uliposema unaanza, mwanzo ulimaanisha MWANZO, (kitabu cha mwanzo kwenye biblia). Lock  akaondoka zake …..

Na mimi naanzia ‘mwanzo’, lakini haitakuwa mwanzo kama ya Eko msije mkaondoka … ila nitapita kwa nukta moja ama nyingine kwenye kitabu cha biblia pia.

Karibu jamvini tupo darasani na mwalimu kesha fika.

Wednesday, April 11, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? Season Finale, Ep1 (Tunabisha hodi Mlangoni kwa Mwalimu wa Walimu Wetu..



Kwenye mfululizo wa Makala hizi, kwenye season 1 na 2, juhudi kubwa imefanyika kuonesha kwamba, kabla historia tunayo ijua haijaanza kuandikwa palikuwepo na jamii iliyo ishi na iliyo endelea kwenye nyanja zote unazo zijua, kwa maendeleo makubwa ambayo leo kwenye karne ya ishirini na moja, ya sayansi na teknolojia hatuja ‘ota’ kuyafikia!

Saturday, April 7, 2018

KUBAKI AU KUHAMA?

GUYS NIMEKUWA KIMYA MUDA KIDOGO, KUTOKANA NA HITILAFU ZA KIUFUNDI, HASA 'SECURITY' ESSUE ZA KIMTANDAO KWENYE BLOGGER YANGU, NA NAONA GOOGLE HAWANA USHIRIKIANO KABISA KWENYE HILI.

NAFIKIRIA KUHAMIA PLATFORM NYINGINE, LAKINI KWANZA NIKAONA NI VYEMA KUWASHIRIKISHA WADAU WANGU.

UWANJA NI WENU KWA MICHANGO NA MAONI .....

Sunday, March 11, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep15 (Nyayo za Wageni Kutoka Sayari Ya Mbali - Kamera, vinasa sauti, sanaa na ndege za kivita...



Je kunayo uwezekano kwamba kamera na vinasia sauti vilikuwepo katika zama zilizo sahaulika, zama za kale za ngano na hadithi za kufikirika?
Ni uwendawazimu kuuliza swali kama hili, ama sivyo? Lakini kwa ambaye amefuatilia mtiririko wa mabandiko haya ni swali ambalo haliwezi kukwepeka.

Sunday, February 25, 2018

JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep14 (Nyayo za Wageni Kutoka Sayari Ya Mbali - Ndege na safari ya mwezini and beyound...


 Friar Roger Bacon katika kazi  zake aliacha sentesi ya maajabu iliyosemeka hivi, “Vyombo vya kurukia angani kama hivi vilikuwa ni vya zamani sana, na hata sasa katika zama zetu bado vinatengenezwa”

Kauli kama hii kwenye maandishi ya karne ya 13 ni kitendawili kisicho na jibu. Kwanza Bacon anathibitisha kwamba vyombo vinavyo ruka angani ni jambo lililokuwepo katika zama zilizotangulia, lakini zaidi pia kwenye zama zake si kitu kipya, huenda kama tunavyoona kwenye zama zetu kwamba ni kitu kipya, lakini kwenye karne ya 13 hakikuwa kitu kipya.

Hermes au Mercury alivaa ndala na kofia zenye mbawa ambao zilimsafirisha kwa kasi ya ajabu juu ya aridhi na juu ya bahari, lakini hadithi kuhusu Mercury zimerikodiwa kama ngano za kale!
Lakini la kushangaza zaidi ni kuhusiana na  mtawala wa China aliyefahamika kama Shun (2258-2208 KK) ambaye si kwamba tu alitengeneza mashine ya kurukia lakini pia alitengeneza parachute


Mfalme Cheng Tang (1766 KK) alimuamuru Ki-Kung-Shi kumtengenezea chombo kinacho ruka angani. Injinia huyo akamaliza mchoro wake na kutengeneza chombo hicho na kukifanyia majaribio na kusafiri nacho mpaka kwenye eneo la Honan.

Mshairi wa Kichina, Chu Yuan (wa karne ya 3 KK) aliiandika juu ya chombo chake cha angani ambacho kiliruka juu sana juu ya jangwa la Gobi kuelekea kwenye vilele vya barafu vya mlima Kun Lun. Akaelezea namna gani chombo chake kilivyo kuwa hakiwezi kuathiriwa na upepo na vumbi la jangwa la Gobi na namna alivyo tumia chombo hicho kufanya, ‘aerial survey.’

Mwanzoni mwa karne ya nne, Ko-Hung aliandika kuhusiana na Helkopta iliyopo China. Somo kuhusiana na usafiri wa angani lilikuwepo tangu mwanzoni mwa historia kama tunavyo weza kuona neon la Sancrit ‘Vidya’ lenye maana ya kutengeneza na kuendesha vyombo vya angani. Mawazo ya msingi juu ya usafiri wa anga yapo kwenye karne na zama ambazo mjomba Darwin anasema binadam anaishi mapangoni na anawasha moto kwa kutumia vijiti vya mti.

Kitabu cha kale mno duniani kutoka India kinacho kwenda kwa jina la Muhabharata, kinazungumzia kuhusu chombo kinacho ruka angani kilicho tengenezwa kwa mbawa za chuma. Ndege?

Vimana inatajwa kuwa ni chombo ambacho kinayo sehem mbili, juu na chini kwa ajili ya abiria, madirisha, muundo wa ‘dome’ na mapanga yanayo zunguka. Zinaruka kwa kasi ya upepo na kutoa sauti murua. Kama vile wanazungumzia ndege zetu za kisasa. Rubani lazima apitie mafunzo maalum ndiyo akabidhiwe vimana. 

Ndege hizo zilifanya maajabu pia ambayo tunayaona yakifanywa na helkopta zetu leo. Kama vile kusimama angani bila kwenda mbele wala kurudi nyuma. Vimana ziliruka juu sana mpaka kuyapita mawingu na bahari kuonekana kama kabwawa kadogo! Rubani aliweza kuona pwani za bahari na mito inayotiririka kuelekea baharini.

Vimana ziliwekwa kwenye ‘vimana griha’, zilitumika kwa ajili ya vita, safari na michezo. ‘Aren’t we doing the same thing with flight to day?’ Lakini ni kweli taarifa, maelezo na maelekezo haya kutoka kwenye karne na zama zilizoitwa za kiza, kwamba zinaweza kuwa ‘ndoto za mchana’ za muandishi? Au ngano za kale zilizo sahaulika au kweli zilikuwepo ndege, kama jet, helkopta na bombadia zama hizo?

Kunayo aina mbili za vitabu vya kale vya Sanscrit huko India, aina moja imegemea kwenye mambo ya kiroho, kidini na maajabu, hii inafahamika kama ‘Daiva’ na aina ya pili ni ile inayo husiana na taarifa za ‘kisayansi’, 

inafahamika kama ‘Manusa.’ Kwenye ‘manusa’, kuna sura ya ‘Samara Sutradhara’ inayohusiana na mambo ya ‘kisayansi’, kijitabu hicho ndani ya ‘manusa’ kinaelezea namna miambili na thelathini za kutengeneza chombo kinacho ruka angani, namna ya kukiendesha kwa maelfu ya kilometa, namna ya kutua kwa njia ya kawaida, kwa lazima na kwa kulazimishwa, lakini pia uwezekano wa chombo hicho kugongana na ndege wa kawaida huko angani! Kama taarifa hii ni ngano ya kufikirika ya kale, basi hii itakuwa ni moja ya ngano bora kuandikwa kuhisiana na elimu ya nga kutoka kwenye zama zilizo sahaulika.

Vita vya angani, kama tunavyo vifanya kwenye zama zetu, si kitu kipya, kwenye zama za historia zilizo sahauliwa, zama ambazo hazina kumbukumbu yoyote ya binadam zaidi ya ‘mnyama aliyekuwa anajaribu kuyamudu mazingira yake’ kwenye zama hizo vita vya anga, vita vya nyuklia vilipiganwa! Vilipiganwa na binadam yupi? Binadam wa Darwin au mwingine?
Kwenye kitabu hicho cha ‘manusa’ silaha za maangamizi ikiwemo nyuklia vimerikodiwa? 

Hiroshima haikuwa sehemu ya kwanza kupigwa na bomu la Nyuklia na wala Marekani siyo taifa la kwanza kutumia bomu la Nyuklia!
Nyaraka kutoka kwenye Pyramid zinaeleza kuwa moja ya kazi za Pyramid ni njia ya kuelekea kwenye uwanda mwingine. Techonolojia hii sijui kama ‘tumeshaigundua’ au bado tunaijaribu kwa siri kasha baadae tuite uvumbuzi! Egypt, mungu Isis siku zote amekuwa akichorwa ni mungu mwenye mbawa anaye ruka angani au anasafiri kwenye chombo maalum kinacho rukwa angani. 

Dhana ya binadam kuruka angani si mpya, ni ya zamani kama walivyo ndege warukao angani ambao wamekuwa wakimshawishi binadam kufanya hivyo.
Mwanzoni kabisa mwa karne hizoo, binadam na hamu ya kuruka angani havikutofautishwa kama akili na wazo. Binadam aliwaza na alitengeneza ndege katika zama hizo zilizo sahaulika. Kutoka kwa binadam wa kwanza aliyekuwa na wazo la kupaa mpaka zama za mwanafunzi wa ‘mystery Schools’ Leonardo wazo linaonekana kuwa ni moja, michoro, zana, muelekeo na malengo ni mageni katika zama zao, lakini sawia katika zama tofauti na maeneo tofauti kama vile muandishi wa mawazo hayo ni mmoja. 

Wachache wanajua juu ya elimu ya kuruka angani na kutengeneza vifaa hivyo, lakini wanajua pia kuwa elimu , vifaa na zana zake zilikuwepo si tu kwenye zama zao lakini hata zama zilizopita, na wengine wote tupo kizani tunadhani ni uvumbuzi katika ‘zama’ zetu!
Hamu ya binadam wa zama zilizo sahaulika haikuwa kusafiri angani tu, bali kusafiri mpaka kwenye sayari na nyota za mbali! 

Hamu ambayo binadam wa leo bado anayo pia, au ameirithi kutoka kwa mababu zake. Lakini binadam wa leo akijinadi kuwa yeye ndiye wa kwanza kupekeleka chombo angani; kwenye Mars, kumpeleka binadam mwezini, kama kweli alienda mwezini, lakini ukweli binadam wa leo siyo wa kwanza kupeleka chombo angani na kwenye sayari zingine, na huenda akawa anatumia maarifa ya kale mno kutafuta njia ya kufika kwenye Mars, kwa siri lakini, ili aweze kuwadanganya wenzake kwamba yeye ndiye mvumbuzi.

Wahindi waliishi Marekani kwa milenia nyingi, lakini walikuambia ni Columbus ndiye aliye vumbua bara hilo! Wachaga wameishi chini ya mlima Kilimanjaro kwa muda mrefu kadiri tutakavyo weza kukumbuka, lakini ni mzungu ndiye aliyegundua mlima huo, kweli? Kama wanaweza kudanganya kwenye lililo mbele ya uso wako, vipi usiyo yafahamu?



Babilon kuna hadithi iliyo rikodiwa miaka 4,700 iliyopita, hadithi ya Etana inayohusiana na kusafiri angani.
‘Nitakupeleka kwenye kiti cha enzi cha Anu,’ anasema tai. Wakasafiri kwa muda wa lisaa limoja kasha tai akasema: ‘Tizama chini, dunia imekuwaje?’ Etana akatazama chini akaona dunia imekuwa kama kabonde na bahari kama kisima. Kisha wakasafiri tena kwa lisaa linguine limoja, kwa mara nyingine tena Etana akatizama chini, na dunia ilikuwa kama jabali na bahari kama chungu, baada ya saa jingine moja dunia ilikuwa kama tembe ya mchanga na bahari haionekani tena!

Anu kwenye ngano za kale ni moja ya ‘wageni’ waliokuja kutoka sayari ya mbali na ‘kumtengeneza binadam’, zaidi pitia bandiko la ‘NAMTAFUTA MUNGU’ kwenye blogi hii. Hadithi hii ya Etana kutoka Babiloni, ni ngano au ni kweli Etana alisafiri juu ya mgongo wa tai, haijalishi sana zaidi ya kuthibitisha kuwa zana ya kusafiri angani kwa binadam ni ya kale mno, lakini maelezo ya namna ambvyo dunia na bahari zilivyo kuwa zikibadilika kila baada ya umbali Fulani, inatilia mashaka kuita hadithi hii kuwa ni ngano, sababu ndicho hasa tunacho kiona leo karne ya ishirini na moja tunapo kuwa safarini angani, kama hawakusafiri angani ni vipi waliona tunacho kiona leo?

‘Hapa mahala hakuna hewa, utulivu na ukimya wake haupimiki, na kweusi kama weusi wa usiku mkuu’. Maelezo ya namna hii utayapata kwenye hadithi ya wananga wetu wa leo! Lakini huo ni mstari kutoka kwenye kitabu cha kale cha watu wa Egypt kinacho kwenda kwa jina la Book of the Dead cha zaidi ya miaka 3500 iliyopita.

Maandishi ya kimila ya kihistoria ya watu kutoka China wame mtaja mtu aliyeitwa Hou-Yih au Chih-Chiang Tzu-Yu, injinia wa mfalme Yao ambaye alikuwa mpenzi wa mambo ya angani. Mwaka 2309 KK aliamua kwenda kwenye Mwezi kwa kutumia ndege wa chuma. Ndege huyu wa chuma pia alikuwa anajua ni muda gani jua linazama na kuchomoza. Je ndege huyu wa chuma siyo kile tunacho ita ‘space-ship?’
Hou Yih alisafiri kwenda angani na kufika mahala ambapo Jua lilikuwa halizunguki/ halisafiri. 

Kauli hiyo ni maalum sana kwenye elimu ya anga, kwani huwezi kuona / kuhisi au kudhani Jua halisafiri mpaka ukiwa angani, kwenye safari ya kwenye mwangu wa anga, mbali kabisa na uso wa dunia.
Injinia huyu alisafiri na mke wake Chang Ngo, kwenye safari hiyo ya kwenda mwezini, Chang Ngo anasema ‘Mwezi ni kama tufe lenye kung’aa, linang’aa kama kioo kikubwa na kIsha ni la baridi sana, mwanga wa mwezi unatokana na jua’, anasema Chang Ngo.
Ujumbe wa mwanamke huyu wa ki China kwenye safari hii ya mwezini ndiyo inayo shangaza kwenye hadithi hii iliyorikodiwa miaka 4,300 iliyo pita. Taarifa za Chang Ngo kutoka maelfu hayo ya miaka yaliyopita, ndiyo taarifa ambazo leo kwenye karne ya ishirini na moja tunazisimamia kuhusiana na mazingira ya mwezi. Kwamba aridhi au udongo wa mwezini ni kama kioo, na kuna baridi mno kushinda vilele vya barafu za Himalaya!

Je sisi ni wa kwanza kwenda mwezini?
Nani kasema? Taarifa za zaidi ya miaka elfu nne iliyopita, zinatuambia kile ambacho, ‘tumekivumbua’ kwenye karne ya 21. Ni vipi miaka hiyo tunayo iita ya giza kulirikodiwa taarifa zinazo thibitishwa ukweli wake na zama zetu zinazo itwa za teknolojia?

Too buzy, but I will work this work to the end Inshallah .... see yaa ...