Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Friday, August 30, 2013

KWANINI FREEMASON WANAFICHA SIRI HADHARANI?


Freemason wanaficha siri zao hadharani, yaani wanacho ficha wanakiweka hadharani, kweupe, kila mtu aone, lakini ni wachache wanao ona, ni kima kuficha mbao kwenye msitu, au kama wanavyo sema Waswahili, ‘mchawi mpe mwanao amlee,’ alama, majina na maumbo yaliyo fichwafichwa, lakini kweupe hadharani yanakuwa yameandaliwa kwa ajili ya kupokelewa na ubongo wa nyuma ambao hufanya kazi bila idhini ya muhusika, na hii ndiyo sababu vitu hivyo huwa havionekani au kung’amuliwa na wahusika sababu ni vitu ambavyo kwenye macho na kwenye akili vinaonekana kuwa havina maana, lakini haimanishi kuwa kwenye ubongo wa nyuma havijarikodiwa, vipo vimekaa vizuri.

Thursday, August 29, 2013

FREEMASON NA MUZIKI


Sauti ya muziki leo ipo kila mahali, kila kona na uchochoro wa dunia yetu ya leo, watu wengi mno wanasikiliza muziki leo hii, kwa sababu mbalimbali, lakini ni watu wachache mno ambao kiuhakika wanafahamu maana ya mashairi, au sababu ya aina fulani ya mashairi na aina fulani ya ala ya muziki kutumika katika muziki husika.

 Ni wachache mno wanao fahamu athari mbalimbali zinazo oneshwa katika video za miziki mbalimbali, nalo hili ni jambo la kusikitisha mno.

Thursday, August 22, 2013

USHIRIKI WA VYOMBO VYA HABARI KUSIMAMISHA NEW WORLD ORDER


“Katika kipindi ambacho ulimwengu umezamishwa kwenye ujinga na uwongo, kusema ukweli ni tendo la kimapinduzi” (George Orwell)

Vyombo vya habari vya kimataifa, kama TV na Magazeti, ‘vyombo vya freemason’. Haviwakilishi chochote zaidi ya maono ya wamiliki wake, freemason, illuminanti na juhudi za waziwazi za kuuzamisha umma katika ujinga, umbumbu, ubususa na upumbavu.

Wednesday, August 21, 2013

TAFSIRI YA MOTO, MWENGE KWA FREEMASON


Baada ya raisi Kennedy kuuwawa mwaka 1969, Scottish Rite Freemasonry, walisimamisha mnara, ‘obelisk’ Dealey Plaza na juu yake wakaweka ‘moto wa kimasonia’ (mwenge). Lakini kama hilo halitoshi kwenye kaburi lake wamewasha moto ambao unawaka mpaka hivi leo, ‘eternal flame’.




Juu ya Pont de L’Alma, mahala ambapo Malkia Diana aliuwawa baada ya gari yake kugongezwa kwenye nguzo ya 13, Illuminanti wamesimamisha hapo ‘moto wa dhahabu wa kimasonia’, (mwenge). Mwenge huo umesimamishwa juu ya nyota yenye ncha tano.

Tuesday, August 20, 2013

NAMBARI 13 INAVYO WEKWA HADHARANI KWA KILA MTU KUONA

Freemason huficha vitu vyao hadharani, kweupe pee, lakini ni wachache ndiyo tunao weza kuona, post hii inazungumzia namna ambavyo nambari 13 inavyo fichwa hadharani.

Katika mifumo mbalimbali ya mahesabu na utunzaji wa taarifa kuna kitu kinacho fahamika kama ‘CODE’. Hii huwa ni muunganiko au mwingiliano wa tarakimu, nambari, herufi na alama nyinginezo, inaweza kuwa vyote hivyo kwa pamoja au kimoja kati ya hivyo katika mpangilio maalum unao fahamika na mmiliki wa code hiyo.
Iliyo nyepesi kabisa katika hili ni ile code ya kutumia herufi kwa tarakimu ambapo herufi inapewa thamani ya tarakimu. Herufi A ni sawa na nambari 1 na kuendelea Z inaishia na nambari 26

Monday, August 19, 2013

MIPANGO YA KISHETANI NA NAMBARI 13

·        Mei 13, 1914 – Bikira Maria aonekana Fatima (Naastaajabu kama haya hayakuwani ni majaribio Project Blue Beam)


·        Mei 13, 1941 – Stalin aliigawa Urusi katika maeneo 7 kwa maandalizi ya vita.


·        Mei 13, 1981 – Jaribio la kumuua Papa lafanyika.

·        Mei 13, 2000 – Sehemu ndogo ya siri kuhusiana na jaribio la kumuua  Papa la mwaka 1981 yatolewa.


·        Mei 13, 2000 -  Papa azungumzia juu ya mnyama atakaye tokea baharini, mnyama mwenye vichwa 7 aliyetajwa ndani ya ufunuo. Kumbuka jina mnyama linayo maana zaidi ya moja, na moja wapo ikiwa ni 666.

Saturday, August 17, 2013

NAMBARI ZA MAAFA ZA KIMASONIA 13 na 33

Unapo wapekua freemasons, marais wa Marekani, mfumo wao wa utawala, kila mara utakutana na nambari hizi, 13 na 33. Wale wanao itwa waanzilishi wa taifa ka Marekani ni Freemason na karibu wote wa maraisi wa taifa hilo ni freemason isipokuwa wachache.



Nambari 3,7,9,11,13,33,39 na jawabu ya kule kinacho patikana kwa kuzidisha nambari hizo kwa nyingine, zote hizo zinayo maana mahususi kwa Illuminanti. Tizama asasi ya siri ya Bilderberg Group inayo wanachama wakuu 39 ambao wamegawanywa kwenye makundi 3 yenye wanachama 13 kwa kila kundi. Wanachama wakuu 39 wapo chini ya Policy Committee yenye wajumbe 13. Wajumbe 13 wa Policy Committee wapo chini ya Round Table of Nine (9). Unafahamu kwamba idadi ya asili kwa majimbo ya Marekani ni 13. Katiba ya Marekani imegawanywa katika vifungu 7 na ilisainiwa na wajumbe 39 wa baraza la katiba” Secret Societies / New World Order" by Milton William Cooper

Tuesday, August 13, 2013

HATUA NNE KABLA YA UJIO WA MASIHDAJJAL/KRISTO WA UWONGO/MPINGA KRISTO/666


PROJECT BLUE BEAM

Waandishi wawili wa habari waliokuwa wakifuatilia sakata ya hichi tunacho kizungumzia hivi sasa au maarufu kama Blue Beam wote wawili walikutikana wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’ ingawa kwenye historia yao hawakupata kuwa na magojwa ya moyo. Vifo vyao vilitofautiana kwa wiki kila mmoja.

Sege Monast alikuwa ni mwandishi wa Internationa Free Press Canada, huyu ni mmoja kati ya waandishi wawili walio kutwa wamekufa kwa ‘ugonjwa wa moyo’.

Moja ya wadau wanao isimamia Project Blue Beam ni NASA, na mradi huu umegawanywa katika sehemu nne ambazo zitafanikisha kuisimamisha New World Order na Masih Dajjal/Kristo wa Uwongo akiwa ndiye kiongozi wa serikali hiyo.

Tuesday, August 6, 2013

HAKI ZA WANAWAKE NA VITA DHIDI YA FAMILIA ...


Haki za wanawake, za watoto na zile za mashoga ni moja ya mfano mzuri wa namna ambayo Illuminanti wanatumia kuishika jamii yetu.

Kwa miaka michache hivyo, tkribani miaka 40 tangu kampeni hizi zilipoanza, wanawake wengi wamepoteza njia yao ya asili na lengo lao mahususi na muhimu katika jamii. Matokeo yake ni kwa familia kusambaratika, ngono holela kuongezeka, kuwa na idadi kubwa ya watoto wa zinaa na idadi ya watu kiujumla kupungua.

Sunday, August 4, 2013

BALAA LA PICHA ZA NGONO NA KIZAZI CHETU

Kwa sasa filamu za ngono zinafanya kazi nzuri sana katika kile tunachoweza kukifananisha na ‘MIND CONTROL’ kama hufahamu msamiati huo unayo maana gani basi nenda kagoogle, na utapata somo.



 Masaa yote sasa tunafikiria ngono, na kila kazi yeyote ya sanaa inayofanywa haijakamilika kama ndani yake haijakuwa na maudhi ya ngono, mavazi hayajauzika kama hayajabeba dhana ya ngono, ilimradi hakuna kinachoweza kufanyika bila kuwekwa viashiria vya ngono, si kwenye siasa, wala kwenye dini, si kwenye utamaduni wala kwenye sanaa. Ni kana kwamba jamii yetu imegundua kitu kipya.

Thursday, August 1, 2013

FREEMASON WANATUMIA FILAMU ZA NGONO NA USHOGA DHIDI YA FAMILIA



SAMAHANI POST HII HAITAKUWA NA PICHA NYINGI KAMA ZINAVYOKUWA POST NYINGINE....

Moja ya madhara makubwa ya luninga kwenye majumba yetu ni ‘kutuprogramu’ sisi watazamaji. Luninga ni zana kama ilivyo zana yeyote ile, na zana si mbaya, ila ni vipi zana hiyo inatumika, hapo ndipo palipo na matatizo. Nayo luninga imekuwa ni zana nzuri sana inayo tumiwa na maadui zetu kutuelekeza kule wanapo pataka wao.
Inautengeneza ufahamu wetu upya juu ya mambo mbalimbali, tunaita ‘brainwashing’ , tunakubaliana na kile kinacho oneshwa kila siku kwenye luninga yetu.
Kati ya mengi ambayo jamii ya leo au kizazi cha sasa tunachoaminisha katika luninga zetu na mitandao mingine ya habari ni kuwa ‘MAPENZI NI NGONO’
 Dada zetu wanajihisi wao si chochote wala lolote, si wakamilifu kama hawatofanya au kuonesha kile ambacho wanakiona kwenye vipindi mbalimbali vya luninga. Lakini mwisho wa siku gharama tunayo lipa kutikana na haya yote ni kuchanika chanika kwa familia na ndoa zetu.