Bahati mbaya sana kwa wakazi wa dunia kila mpango wa uliofanywa na maadui zetu unakwenda kama wanavyo taka wao, New World Order iko wazi, lakini ni kwa wale walio huru kiakili ndiyo wanayo weza kuiyona, wengine tunasubiri itangazwe rasmi. Lakini nikipi hicho kilichoko kwenye New World Order?

Mpango mchafu, mweusi mbaya na hata usiofikirika kwa mtu wa kawaida ni KUPUNGUZA idadi ya watu duniani kwa asilimi 90! Iliasilimia 10 itakayo baki iwiane vizuri na mazingira yake. Kwa kutumia njia mbaya na kushinda mnyama. Hapo utakutana na Nyota ya Kijani, Mpango wa uzazi salama, elimu ya ngono mashuleni, vyakula na madawa yanayotiwa dawa na visababishi vya ugumba kwa siri, virusi na maradhi ya kutengeneza maabara kama ebola, ukimwi, chanjo za aina kwa aina, vita kila kona ya dunia na mapango wa WWIII, ukame na majanga mengine ya kutengeneza tunayo dhani ni ya asili.

Kisha idadi ya watu inayotakiwa ikisha fikiwa ajenda itawekwa hadharani ikiwa na Serikali Moja ya Dunia (Serikali ya Kishetani), Dini moja kwa watu wote (Dini ya Kumuabudu Shetani) Jeshi Moja la Dunia (Kwa ajili ya kupambana na wale watakao taka kuipindua serikali hiyo) Sarafu moja kwa dunia nzima, na wananchi wote wakuwa na Microchip kwa ajili ya kufuatilia nyendo za kila raia masaa 24/7.

Kifupi ni kuuwa asilimia 90 ya binadamu wote, na kutawala nyanja zote za maisha, na kumtawala kila mtu na kila kitu kutoka siku unazaliwa mpaka unaingia kaburini!

Wakati unafikiri hilo haliwezekani mpango huu umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 90%

NAIKUBALI HII

NJIA YA MATUMAINI KWA TEJA WA PORNOGRAPH

Hichi ndicho anachokisema Mwanasaikriatiki wetu Norman Doldge, “Ukurasa wa nyuma kwenye jarida la wanaume liitwalo Risque na kuras...

Saturday, May 25, 2013

JE KANUMBA ALIWAHI KUWA NI FREEMASON? Part II


TUENDELEE NA SEHEMU YETU YA PILI YA HADITHI YETU ...


JE HILI LINATOSHA KUMFANYA KANUMBA AWE NI FREEMASONRY? KWA SABABU ALIKUWA MAARUFU, ALIKUWA NA KIPAJI, ALIKUWA NA MVUTO KWENYE JAMII NA ALIKUWA NA USHAWISHI WA KIPEKEE KWENYE JAMII KUTOKANA NA KAZI ZAKE, JE HILI LINAWEZA KUMAPATI HIYO TIKETI YA UMASONIA?


Thursday, May 23, 2013

JE KANUMBA ALIWAHI KUWA NI FREEMASON?

HII NI MOJA KATI YA HABARI NYINGI ZILIZO JARIBU KUMFUNGANISHA KANUMBA NA UFREEMASO,


JE KANUMBA ALIWAHI KUWA NI FREEMASON?

Kumekuwa na wimbi kubwa la watu maarufu hapa nchini kuhusishwa na mtandao wa freemason. Wanamuziki kadhaa wamekuwa wakihusishwa na jamaa hawa. Kifo cha Kanumba nacho hakija achwa nyuma kwenye hili, inasemwa naye alikuwa ni freemason na hata kifo chake chenyewe kimekuwa kikitajwa na baadhi ya watu kuwa kimesababishwa na freemason. Ama habari hizi zimekuwa siyo rasmi, kutoka kwa baadhi ya watu maarufu hapa nchini  kuhusishwa na freemason mpaka Kanumba na kifo chake.

Tuesday, May 21, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI? Part V



Tunaendelea na safari, lakini leo tunatizama kwaenye upande wa KUPUNGUZA IDADI YA WATU


Wananchi hawawezi kusimama tu na kuwaachia watu wengine maaisha yao wayatawalie, kabisa
“Kama ningeweza kurudi tena duniani baada ya kufa, ningependa nirudi duniani kama kirusi kinacho uwa, ili niweze kuuwa watu na kupunguza idadi ya watu duniani. “– Prince Philip, Duke wa Edinburgh.
I dadi ya watu duniani ni kubwa mno kutokana na maelezo ya maadui zetu. Suluhisho lake ni kuwa wameandaa mpango ambao utahakikisha idadi hii inapungua na kuwiana na malengo yao.
Kunazo njia nyingi na mipango ambayo nafanyiwa kazi na kutekelezwa kikamilifu na maadui zetu ilikuweza kukamilisha mpango mzima, mipango hiyo inalenga kupunguza idadi ya watu na kufikia bilioni 2 mpaka milioni 500 ikiwezekana kutoka kwenye idadi iliyopo sasa ya watu bilioni 6-7.
Zipo njia kuu tatu ambazo maadui zetu wamekuwa wakizitumia kufikia malengo yao ya kupunguza idadi ya watu. Moja ni mazingira hasi ya kiuchumi na kijamii yanayo tengenezwa kwa kupitia serikali za kitaifa na mashirika ya kimataifa, mazingira hayo yanapelekea kuwepo kwa ukame mkubwa, upungufu wa chakula na njaa kwa kiasi kikubwa na kwenye maeneo makubwa ya watu. Taktibani watu milioni 40 hufa kwa njaa kila mwaka. Na hivi karibuni shirika la chakula duniani limetangaza na kuwashauri watu kuwa inafaa BINADAMU SASA KULA WADUDU KWASABABU HAKUNA CHAKULA.


Sunday, May 19, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI? Part IV

VIPI WAPENDWA WANGU, TUNAENDELEA TENA NA HADITHI YETU YA KUSISIMUA, LEO KATIKA SEHEMU YA NNE YA MTANANGE HUU TUTATUPIA JICHO MBINU CHACHE ZINAZO TUMIWA NA MAADUI ZETU KUFANIKISHA MPANGO WAO KAMAMBE DHIDI YETU ...


Wananchi hawawezi kusimama tu na kuwaachia watu wengine maaisha yao wayatawalie, kabisa haiwezekani kuona hilo linatokea, labda jambo hilo liwe linafanyika kwa namna ambayo binadam wenyewe hatulielewi. Sehemu ya ajenda hii ya kuwatawalia watu imewekwa kwa namna ambayo wanachi wenyewe, wanasukuma gurudumu la kuelekea kwenye kituo cha kuuza uhuru wao kwa hiyari. Kiuhakika kila tunapo peleka fedha zetu benki, ni kama tunawapatia maadui zetu nguvu zaidi uwezo wa kuendelea kutupora uhuru na mali zetu. Wametufanya tuamini kuwa si kwamba tu sisi hatuwezi kufanya chochote bila wao, lakini kile ambacho ni kizuri kwao ni kizuri kwetu pia.

Illuminanti pia wanatumia mianya na kutengeneza matukio ya kutisha kwa ajili ya kuendeleza au kutengeneza mazingira ya kufanikisha ajenda yao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutumia mbinu kama vile ‘PROBLEM-REACTION-SOLUTION’ na nyinginezo ambazo tuatazitupia jicho hapa.

Mathalani, njia ile ya Preoblem-reaction-solution, huwa inafanyika kwa namna ifuatayo, wanatengeneza tatizo, au wanalikuza tatizo kupitia vyombo vya habari au kwa kutokufanya chochote tatizo linapo tokea. Kisha baada ya hatua hiyo wanatumia vyombo vyao vya habari kuweka mazingira amabyo yatapaza sauti ya kutaka kuwepo na suluhu ya tatizo. Lakini suluhu ambayo wao walisha iandaa kabla ya tatizo kutokea, na wanacho fanya sasa ni kurubuni maawazo ya watu kukubaliana na suluhu hiyo. Kisha baada ya hatua hiyo ya kurubuni mawazo ya watu, kinacho fuata sasa ni kutekeleza suluhu ambayo wao wameipendekeza kwa wananchi na imeonekana kukubalika, lakini kinacho fanya suluhu hiyo ni kuwaongezea wao nguvu na madaraka zaidi juu ya maisha yetu ya kila siku, Mfano mzuri wa njia hii ni 9/11 ambayo baada ya hapo kilicho fuata ni VITA DHIDI YA UGAIDI.


KILA LEO, KILA AINA YA USHAHIDI UNAZIDI KUMIMINIKA AMBAO UNAPINGANA NA HADITHI YA SERIKALI YA MAREKANI, AMBAO UNASEMA NI UONGOZI WA BUSH MWENYEWE NDIYO ULIOSHUGHULIKIA NA KUFANIKISHWA KULIPULIWA KWA MINARA HIYO MIWILI, PENTAGON NA BUILDING 7.

NJIA NYINGINE WANAYO TUMIA MAADUI ZETU NI ‘FALSE FLAG OPEREATIONS’
Hii ni njia nyingine kali sana ya kurubuni mawazo ya watu na kuyapeleka kule ambako maadui zetu wanapo pataka, njia hii hutumika kufanya uvamizi, uhalifu na uharibifu kwa kutumia ‘NEMBO,’ ‘BENDERA,’ au ‘ALAMA YA ADUI YAKO’ Ilikuweza kupotosha jamii kuwa ni adui yako ndiye aliyefanya hivyo, ni adui yako ndiye aliyevamia pale, wakati KIUHAKIKA NI WEWE NDIYE uliyefanya hilo. Aaina hii ya mbinu huwawezesha maadui zetu kuweza kupora malighafi, kutengeneza faida kubwa kutokana na vita, na pia kutupora haki na uhuru wetu. Mfano wa mbinu hii ni,

Thursday, May 16, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI? Part III


            WAPENDWA MTANANGE WETU BADO UNAENDELEA, MTANIWIA RADHI NINAPOSHINDWA KUPOST KWA WAKATI, HII NI KUTOKANA NA MAJUKUMU MENGINE YANAYO NI BANA, LAKINI TWENDE PAMOJA...... TUNAENDELEA TULIPOISHIA JANA ... 

             Leo hii, N.M Rothschild & Sons ni benki ya kuu ya uwekezaji ambayo ipo nje ya London. Ni moja kati ya 10 bora benki za uwezeshaji duniani. Mwaka 2007 benki hii iliweza kutengeneza faida ya kiasi cha dola bilioni 566. Hicho ni kile kinacho fahamika kama ‘taarifa rasmi’ lakini wanazo benki duniani kote, ambazo zinawawezesha kuwa na maamuzi ya kiuchumi kote duniani.

             Rockefellers wanamiizizi mirefu ndani ya Marekani, walianza kwenye karne ya 19, kwa msaada wa fedha toka kwa JP Morgan ambaye naye aliukwaa utajiri huo kupitia kwa ushawishi wa Rothschild. John D. Rockefeller alipewa fedha hizo kwa ajili ya kazi ya kusimamia na kuendeleza malighafi zihusianazo na mafuta.
Rockefeller fedha zao nyingi zinafichwa kwenye taasisi mbalimbali za kijamii walizo anzisha na ambazo zina majina na maaudhui ya kusaidia jamii, kama vile The Rockeffeller Foundation.

             Mwaka 1913 The Rockefeller Foundation ikawa moja wa wadhamini wakubwa kwenye tafiti za utabibu. Iliwachagua wanasayansi na madaktari ambao walionekana wanafaa kudhaminiwa kwenye tafiti hizo. Msisitizo ulikuwa ni kwenye madawa namna gani madawa yanafanya kazi mwilini na namna gani mwili unapata athari kutokana na madawa hayo. Tafiti hizo zikarudishwa vyuoni, hasa vyuo vya udaktari na kuwapatia madaktari matokeo ya tafiti hizo, yaani aina ya dawa zilizo patikana, nazo ziwe kwa ajili ya kutibu watu, LAKINI KILA MWENYE AKILI HAAMBIWI TIZAMA, LEO NI DAWA NDIYO ZINAZO UWA WATU. Mpaka leo tafiti hizo bado zinaendelea. Aina hii ya hadithi tuipata katika kila Nyanja au sekta ambazo ‘aina hizi’ za mashirika zimeweka fedha zao.

Wednesday, May 15, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI? Part II


Hadithi ya Illuminanti ya kutawala ulimwengu wote ni ya kale mno kama ilivyo historia ya binadam mwenyewe, ni kwenye historia hiyo na njama hizo kuliko pelekea kuwepo na kile kinacho fahamika kama ‘BENKI KUU’ katika kila kona ya dunia- ambapo ni watu wachache Fulani wasiyo fahamika kwenye macho na masiko ya wanajamii wengine, ndiyo wanao tengeneza ‘FEDHA HEWA’ kwa kuwakopesha watu kwa riba, kwenyenye mfumo huu wa benki ndipo ulipo uti wa mgongo wa BABILON BROTHERHOOD, AMBAPO BENKI ZINAKOPESHA FEDHA AMBAZO HAINA NA KUCHAJI RIBA KWENYE GEDHA HIZO.

Monday, May 13, 2013

FREEMASONRY WANAFANYA NINI NA MALENGO YAO NI YEPI?

Swali la kuwa Freemasonry wanafanya nini na malengo yao ni yepi, ni swali lenye jibu kepesi sana lakini lenye maelezo marefu n kwa kina chake.

Freemasonry lengo lao kuu ni kushirikiana na asasi zingine za siri kusimamisha utawala wa kishetani ulimwenguni kwa mataifa yote na watu wote duniani. Freemasonry wanacho kifanya sasa ni kushughulikia maono hayo kuona yanatimia kwa kiwango chake.

Kwa ufupi sana hayo ndiyo malengo na ndicho wanacho kifanya freemasonry.

Lakini kama nitaachia hapo inamaana kuwa msomaji unaweza kukubaliana na mimi ama la, unaweza kukubaliana na mimi kwa maana ya kuniamini kwa hayo niliyo yaeleza au kutokukubaliana kwa maana ya kutokuamini hayo niliyo yasema.

Lakini kwa muda mrefu sana maana na maudhui ya kazi zangu binfasi katika kuwaelimisha watu juu ya hili nimekuwa nikiepuka dhana ya kumfanya msomaji wangu AAMINI kile nilichoandika, bali kumuwezesha msomaji wangu KUELEWA kile nilicho andika. Kwa maana hiyo basi madai mawili niliyo yaeleza hapo juu ndiyo yatakuwa dhana kuu ya blogu hii, kukufanya UELEWE, malengo na kazi za freemasonry kwa kina. Hivyo kwa kiasi kikubwa sana kazi zitakazo fuata baada ya hapa ni kuelezea mambo hayo mawili kwa mapana yake.


MOYO WA FREEMASONRY NA WASHIRIKA WAKE NI KUICHUKUA DUNIA YOTE NA WENGINE TUWE WATUMWA

MUUNDO WA PIRAMIDI LA KIUTAWALA LA FREEMASONRY


Hayo kiuhakika ni madai mazito sana niliyo yaandika hapo dhidi ya freemasonry,

 Kwamba hii dunia tunayo ishi sasa, ambayo kila nchi inayo kiongozi na mtawala wake, serikali na wafanyakazi wake, taasisi za kiserikali na mashirika yake, kwamba UTAWALA HUO SIYO UNAO TAWALA DUNIA HIVI SASA, AU SERIKALI HIZO SIZO ZILIZO NA MAMLAKA YA NCHI ZAO NA DUNIA KWA UJUMLA .....

SWALI NI NANI HAO WENYE HAYO MAMLAKA??????????


Saturday, May 11, 2013

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part III


Hata hivyo kulikuwa na madhehebu mengine ya watu walio fahamika kama Essenes, hawa nao walikuwa ni Wayahudi, mafunzo yao hawa nayo yanakuja kuwa ni sehemu muhimu ya mafunzo na muongozo kwa Illuminati na freemasonry katika historia yao yote. Essenes katika picha hii wana uzito wa kipekee, kwa vile ni kutoka kwao ndiyo freemasonry wanajivunia walivyo navyo. Ingawa Essene walipatikana Palestina zaidi lakini mafunzo yao yalienea mpaka Egypt. Essene hawa walikuwa ni moja kati ya madhehebu makubwa matatu ya Kiyahudi katika dini hizi za kipagani, wengine walikuwa ni Pharisees na Sudducees. Essene walitambulika kama warithi wa mafundisho ya Chaldea, elimu ya nyota ya wa Misri, na elimu ya tiba ya wa Persia wa kale, wali fananishwa na makuhani wa Magi kutoka Persia.


Kwa msaada wa mitume waliofuata hekalu lilijengwa upya, lakini likaja kubomolewa tena kwa mara nyingine na Wayahudi kubakizwa kwenye dini za kipagani za watu wa Roma.

Hivyo mafunzo haya ya kipagani yaliwatoa kabisa Wayahudi katika imani ya Mungu Mmoja na kuwaingiza katika imani za kishirikina ambazo ndani yake shetani aliabudiwa waziwazi.
Quran nayo ikalitaja hili kuhusiana na Wayahudi na athari waliyo ipata baada ya kutekwa na kupelekwa Babyloni.


Wednesday, May 8, 2013

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part II


Kuna vyanzo vingi vinavyo elezea kuwepo kwa freemasonry Kabbala ya 1717, vyanzo hivyo ni vingi, vinahitaji muda na uyakinifu ilikuweza kutofautisha baina ya almasi na vipande vya vioo. Kuna vilivyo andikwa kwa nia nzuri tu, kuna vilivyo andikwa kwa ajili ya kupotosha, na kuna vilivyo andikwa na wale wasio fahamu wanacho andika, lakini wote wakijaribu kuthibitisha au kukanusha kuwepo kwa freemasonry kabla ya 1717.

Katika mtandao wa Bible Beliver, wameweka hadithi moja nzuri sana ya namna ambavyo freemasonry walivyo kuwepo kabla ya 1717, napo hapo nitaiangalia kwa uchache sana, kwa urefu hadithi hii unaweza kuitizama mwenye hapa. http://www.biblebelievers.org.au/masonry2.htm

Hadithi yenyewe inazungumzia habari ya mwaka 43, kipindu kifupi sana baada ya Yesu/Kristo (Issa Mwana wa Mariam Rehma ya Mungu iwe juu yao wote) alipo paishwa kwenda mbinguni. Ulitokea mtafaruku baina ya waumini wa dini za kipagani na dini aliyoiacha Yesu. Jamii ilikuwa imechanika chanika mno. Baba anamakana mwana, mwana anamkana baba, mama na baba hawaelewani, dada na kaka na ndugu wengine halikadhalika. Uadui mkubwa umeletwa na kile kilicho onekana kama ‘dini mpya’.

Waliyo zikataa ‘dini mpya’ alikuwemo mtu aliyeitwa Mfalme Herod Agrippa II, anatajwa kama alikuwa ni kibaraka wa dola ya Roma, na Wayahudi walinyanyasika vibaya kwenye mikono yake, hasa pale walipo itikadi kuwa Yesu ni mtume wa Mungu Mmoja na wao wanayafuata mafundisho yake.


Mfalme Herod Agrippa II
 Mfalme Herod alisimama mbele ya baraza la Jerusalem na kulihutubia juu ya zahama au kisu kilicho ichana jamii yao, juu ya mafundisho ya ‘dini mpya’ na namna gani watasimama dhidi ya dini hiyo, na wafuasi wake na mafundisho yao, ili nyumba za Jerusalem zisalimike na ‘balaa’ lake.

Katika baraza hilo mfalme alikutana na watu tisa tu (9), hii namba itizame na ikumbeke vizuri, tutakutana nayo huko mbele na kasha nitakueleza maana yake hasa nini. Waheshimiwa tisa walio kuwepo kwenye baraza hilo ni Herod Agrippa II, Moab Levy, Adoniram, Johanan, Jacob Abdon, Antipas, Solomon Aberon, Ashadi Abia, na Hiram Abiud.

Mfalme Agrippa akawambia kwanza hakubaliani na Yesu kwamba ndiye Kristo, kwa vile yeye na wenzake na mababu zao kunayo Kristo mwingine waliyekuwa wanamngojea, ambaye ndiye atakuwa KING/Mfalme wa Jerusalem, na sasa hivi kiti chake kipo kinamngojea, kama tunavyo jua harakati hizi za kuwa na kiongozi mmoja duniani kote, serikali ya kiongozi huyo itakuwa ni Jerusalem na hapo tumemuona Agrippa miaka hiyo akizungumzia kitu hicho, hicho, na leo hii tunawaona freemasonry wakiandaa makazi ya mfalme huyo, na kumbuka kwenye hadithi ya Mtume Muhammad (s.a.w) kuwa Dajjali, Mpinga Kristo, au huyo Kristo ambaye Mfalme Agrippa anayemtaja, atauwawa katika eneo linaloitwa ‘Baab Lud’ leo panajulikana kama Tel Aviv, hapo ndipo Dajjali atakapo uwawa, kwa vile ni ndani ya Jerusalem ndipo atakapo taka kusimamishia dola yake na ukitizama matukio ya kiulimwengu leo ndicho hasa Illuminati wanacho kiandaa, kitu cha mfalme mwenye jicho moja.

Saturday, May 4, 2013

FREEMASONRY ILIANZIA WAPI Part I





Freemasons ni jumuiya ya kale mno, lakini kabla ya 1717 haikuwa ikifahamika rasmi kama Freemasons, ni kiuhakika FREEMASONRY walikuwa ni waashi ambao walikuwa na utaratibu wao wa namna ya kufanya ujenzi wao, walikuwa huru katika Ulaya ya zama za kati wakiruhusiwa kuzunguka kila mahala kote duniani kama wangeweza, hawakuwa watu ambao wakijihusisha na mambo ya maajabu kama wanavyo fanya Freemasons wa sasa, mpaka pale mafundisho ya kipagani na uchawi kutoka Mashariki ya Kati kupitia kwa Knights Tampler yalipochomokwa kwenye asasi hii ambayo awali haikujua chochote zaidi ya ujenzi.
Hawa wajenzi wa zama za kati ndani ya Ulaya walifahamika kwa jina la kazi yao, yaani masoni au kwa lugha yetu fundi mwashi. Masoni walikuwa na utaratibu maalum wa kulinda siri hizi zinazo endana na kazi yao, walikuwa na mahekalu yao, ambapo humo wanajumuiya walifundisha maajabu na siri za kazi zao za ujenzi, lakini haya hayakufunuliwa kwa mtu baki. Hivyo majengo mbalimbali ya ibada zama hizo, majengo ya kiserikali, makasiri ya kifalme na nyumba za watu binafsi wenye ushawishi wa kiuchumi katika jamii zilijengwa na watu hawa, masoni. Hii ndiyo maana Ulaya ya zama hizo haikunufaika na maarifa haya kwa haki yake kwa vile haikuwa elimu aliyo pewa kila mtu, bali ni kwa watu maalum na walitumia kwa majengo ya watu na vikundi makhususi. Siku zote Freemasons walicho nacho ni cha kwao na ulicho nacho pia wanataka wakichukue, daima wako kinyume na jamii inayo wazunguka, hivyo lolote la kuinufaisha jamii halielezwi kwa wanajamii na wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanajamii hawayapati maarifa hayo. Desturi hii wako nayo mpaka leo hii, kila shida unayo iona duniani au maradhi ujue kuna tiba yake, kuna tiba ya kansa, kuna tiba ukimwi kutaja kwa uchache, kuna suluhisho juu ya tatizo la uchumi, kuna suluhisho juu mmomonyoko wa maadili lakini katu hayatatolewa, kwa sababu wewe unaye soma kitabu hichi ndiye adui yao nambari moja!


Moja ya masalio ya majengo yaliyo jengwa na MASONI wa zama za kati na ambayo pia lilitumika kama ofisi yao.

Masoni hawa wa zama za kati katika mahekalu yao walihifadhi zana zao za kazi, walipumzika humo na pia kula chakula humo. Katika mahekalu hayo wanajumuiya walisimikwa katika madaraja ya kimasoni, zama hizo kulikuwa na madaraja matatu tu, yaani Apprentices, Journeymen na Grandmaster. Mason, hawa walikuwa wakijikusanya kama kikundi cha ushirika ili waweze kupata kazi husika, walitambuana kwa salamu zao za siri na ishara mbalimbali zilizo kuwa hazifahamiki kwa watu wengine.


Wednesday, May 1, 2013

WAO NI AKINA NANI?


FREEMASON NI AKINA NANI?
Swali hili limekuwa likiulizwa na mimi binfsi mara kadha tangu na baada ya kuanza kuchapisha makala zangu kwenye gazeti la Mtanzani, nimekuwa nikiulizwa swali hili. Ni swali ambalo muulizaji hulidhani ni jepesi tu na lenye majibu ya haraka haraka, lakini ukweli ni tofauti kabisa.

Kwanza kubaliana na mimi kuwa tunao freemason wa aina mbili kote duaniani. Kuna jumla ya wanamasonia wanao karibia milioni sita kote duniani, ambao kama nilivyo sema tunaweza kuwagawa katika makundi mawili tu.
 Kundi la Kwanza ni Freemason wanao onekana (Visible Freemason)
 Kundi la Pili ni Freemason wasio onekana  (Invisible Freemason)

Asilimia tisini na tani mpaka tisini na nane (95-98%) ya freemason wote duniani wapo kwenye kundi la pili 'Visible Freemason' na Asilimia tano mpaka mbili (2%) ya freemason wote ni Invisible freemason.

Hivyo basi mpaka utakapo yaelewa makundi haya mawili ya kimasonia ndipo utakapo weza kuja na tafsiri sahihi au definition ya freemason.

FREEMASON AMA KATIKA LUGHA YETU 'WAJENZI HURU'

HII NI NEMBO KUU YA KIMASONIA


FREEMASON NI AKINA NANI?
FREEMASON NI NINI?
ILIANZIA WAPI?
WANAFANYA NINI?
MALENGO YAO NI YEPI?

JE NI SALAMA NA SAHIHI KUWA MWANACHAMA?

Hayo na mengine mengi ndiyo maswali yanayo waumiza vichwa wana Afrika Mashariki, na hata ulimwengu kwa ujumla, lakini pia kumekuwa na blanketi la kiza kwenye majibu ya maswali na mfano wa hayo, ni kima majibu wanayo yapata walimwengu hayakidhi haja ni kima kuna mabcho hakiwekwi wazi.


Kwenye mfululizo wa machapisho haya kwenye blog yako hii tutachambua maswali hayo na majibu yake kwa kina kadiri nitakavyo weza.


NDANI YA HEKALU LA KIMASONIA